Majira ya joto ughaibuni,almaarufu kama summer huwa yana matukio
mbalimbali yenye kuvutia na yenye lengo la kuwaunganisha wananchi na
hususani watanzania wanaoishi katika nchi mbalimbali ulimwenguni.
Miongoni mwa matukio ya namna hiyo, ni pamoja na michezo.
Katika kuendeleza “jadi” hiyo ya kujidai na kujumuika kunako majira
ya joto, jiji la Toronto nchini Canada linatarajiwa kushuhudia mpambano
wa kukata na shoka baina ya mashabiki wa Yanga na Simba wanaoishi nchini
Canada. Pambano hilo ambalo ni la marudiano linatarajiwa kufanyika
Jumamosi hii tarehe 14 Julai katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Bur Oak
uliopo katika mji wa Markham,Ontario ambao ni mji shirikishi wa eneo
linalojulikana kama Greater Toronto Area(GTA)
Katika pambano la kwanza,mashabiki wa Yanga waliondoka vichwa chini
baada ya kuangukia pua kwa kuchabangwa jumla ya magoli 8-3. Kutokana na
kipigo hicho,Yanga wanasema ni muhimu kwao kulipiza kisasi na kulinda
heshima ya Yanga. Tayari Yanga wameongeza nguvu kwa kuwaingiza kundini
vijana sita ambao wapo chini ya umri wa miaka 20 kwa minajili hiyo hiyo
ya kulinda heshima.
Kwa upande wa Simba,wao wanasema kama ilivyo jadi,ushindi kwao ni lazima na Yanga watarajie kipigo kingine kikali tu.
Waandaji wa pambano hilo wanaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili
kuweza kuunga mkono timu zao wanazoshabikia. Mechi itachezeshwa na refa
kutoka Iran ili kuondoa uwezekano wa “mlungula” na upendeleo.
Friday, July 13, 2012
Monday, August 1, 2011
Saturday, June 25, 2011
Sunday, June 19, 2011
Friday, June 10, 2011
Wednesday, June 8, 2011
Sunday, February 20, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)